Penzi ndizi kisukari ,utamu ni wa zabibu
Umbo lake pisikali , nalimudu husudu
Mwisho wa safari ,kwengineko ni sumu
Huba limemea kwako, wacha nilipalilie
Hana mbio za farasi, mwendo wake taratibu
Utadhani alimasi , ananvyovutia usiku
Tabasamu lake asali, anafuraha kila siku
Huba limemea kwako, wacha nilipalilie
Wendo wangu tausi ,wavutia muhibu
Tena walijua penzi ,kila siku ni karamu
Wendo wangu mlezi, sitaki tena haramu
Huba limemea kwako, wacha nilipalilie
Katu sina wasi wasi, moyo wako uko pangu
Nakupenda mpaka basi ,mi wako weni wangu
Moyo umeupiga pasi, wewe ndiyo my wangu
Huba limemea kwako ,wacha nilipalilie
Hajanishikia hirizi, penzi lake nasujudu
Nimekita kizizi, kucheat kwake kurufu
Katu kwake sitelezi ,amenifunga miguu
Huba limemea kwako ,wacha nilipalilie
Login to join the discussion