Wendo kipenda roho,kakweli umeniweza
Raha ya wangu moyo,kwako nimeipata
Mahaba ni mtiririko,nashindwa kueleza
Hayuni umeninasa,siwezi hata kubwata
Mwali kiuoni ni feni,Fundi yuapepeta
Yale ya unyagoni,kiukweli aliyashika
Siishiwi hamu hani,mtima umenishika
Hayuni umeninasa,siwezi hata kubwata
Akili hazipo hayawani,mi kwako taabaani
Umeniweza yamkini,naugua huba wodini
Nimempata waubani,kwengine nitakeni
Hayuni umeninasa,siwezi hata kubwata
Huyu si kungunguru, kuruka majalalani
Wala sitakufuru,amenibariki manani
Hana mbio za faru,mwendo wake ni tausi
Hayuni umeninasa,siwezi hata kubwata
Login to join the discussion