Hivi alieutunga,hakujua kuna uchungu?
Ama Adam na hawa,walichafua ulimwengu?
Kama kunae anadawa,nipeni basi mwenzenu
Upendo ni ubeti, sijui kautunga nani
Kuna mda nikikaa,najihisi wajana mfu
Ama sina hulka yakuvutia,nawaza sipati jibu
Ama nyota imefifia,mawazo yananisurubu
Upendo ni ubeti ,sijui kautunga nani
Likianza hunoga,asli tende kwa zamu
Vidole nang'a nang'a,utahadhisia utamu
Mgongo kusuguana,kudekezana mahabubu
Upendo ni ubeti ,sijui kautunga nani
Usiku kwa mchana,utapewa dhahabu
Utapewa vya kunona,halua na zabibu
Utasahau kutendwa,uturi huishiwi hamu
Upendo ni ubeti, sijui kautunga nani
Login to join the discussion
¶ Kali sana
Login to join the discussion