Imefika alfajiri,hakika kunapambazuka
Namsikia mwadhini, akiiadhini adhana
Jua linaangaza usoni,nyoyo zina furaha
Kenya liogopeni giza,likirudi tena ni sumu
Siku inanukia udi,sio uvundo wenye kunuka
Kumekucha kila sayari, na ardhi inachibuka
Kumekucha tunatanabahi,giza limetimuka
Kenya liogopeni giza ,likirudi tena ni sumu
Ukumbuke mti uliozaa,ukombozi sikutoa damu
Usianze kubwagaza,nakuukabili ni kazi ngumu
Tusirudi kujilaza,na tukaupoteza ufahamu
Kenya liogopeni giza,likirudi tena ni sumu
Wakenya kumekucha,kukumbuka ni muhimu
Ndege wanatutumbuiza ,siku mpya kuisalimu
lisijekupumbaza,jua akatumia muaji sumu
Kenya liogopeni giza,likirudi tena ni sumu
Login to join the discussion
¶ Wakenya lazima tufungue macho, laa sivyo hatutawai pata mabadiliko ya maana. Kazi safi Chiddy👍
Login to join the discussion